IQNA

Rais wa Uturuki atahadharisha

Vita vya msalaba vinaweza kuzuka baada ya Austria kufunga misikiti, kuwatimua maimamu

14:38 - June 10, 2018
Habari ID: 3471550
TEHRAN (IQNA) – Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amemkosoa Kansela Sebastian Kurz wa Austria kufuatia uamuzi wa serikali yake kufunga misikiti saba na kuwatimua maimamu 40.

Nina wasi wasi kuwa hatua ambazo kansela wa Austria amechukua zitapelekea dunia kukaribia vita vya msalaba na hilali," alisema Erdogan katika dhifa ya futari mjini Istanbul akiashiria uwezekano wa kuzuka vita baina ya Waislamu na Wakristo katika uga wa kimataifa.

Erdogan amesema Uturuki itachukua hatua kufuatia hatua hiyo ya Austria ya kuwatimua maimamu na kufunga misikiti.

Ijumaa Austria ilitangaza kuwa itafunga misikiti saba na kuwatimua makumi ya maimamu na familia zao kutokana na kile inachodai ni mkakati wa kuzuia 'uislamu wa kisiasa' na ufadhili wa kigeni kwa makundi ya kidini.

Herbert Kickl Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya mrengo wa kulia ya Austria, Ijumaa alitangaza mpango wa kuwatimua maimamu  ambao wanafadhiliwa na Uturuki nchini humo. Aidha amesema watu 150 watapoteza haki ya kuishi nchini humo katika oparesheni hiyo.

Kansela wa Austira Sebastian Kurz amewaambia waandishi habari kuwa serikali yake itafunga msikiti unaofadhiliwa na Uturuki katika mji mkuu wa nchi hio, Vienna. Aidha amesema serikali pia imeamua kubatilisha kibali cha Jumuiya ya Kidini ya Waarabu ambayo inasimamia misikiti sita ambayo pia itafungwa. Kansela wa Austria amesema uamuzi huo umechukuliwakuzuia 'uislamu wa kisiasa' na ufadhili wa kigeni kwa makundi ya kidini.

Kurz, ambaye alichaguliwa kuwa kiongozi wa Austria mwezi Desemba katika muungano wa Chama cha Freedom ambacho kinawapinga wahajiri wa kigeni amesema uamuzi huo umechukuliwa baada kuenea picha za watoto wanaosoma katika misikiti inayofadhiliwa na Uturuki wakicheza tamthilia ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia inayohusu mapigano ya Gllipoli.

3466037

captcha