IQNA

Ozil, Mchezaji Mwislamu Mjerumani, amjibu mwanasiasa anayeuchukia Uislamu

14:52 - March 11, 2018
Habari ID: 3471425
TEHRAN (IQNA)- Mesut Ozil mchezaji mashuhuri Mwislamu katika timu ya taifa ya soka ya Ujerumani amemjibu mwanasiasa anayeuchukia Uislamu ambaye alimkosoa kwa safari yake ya Umrah.

Hivi karibuni Alexander Gauland, mwanachama wa chama cha mrengo wa kulia chenye chuki na Uislamu cha Mbadala kwa ajili ya Ujerumani-Alternative for Germany-(AfD) alimkosoa vikali Ozil kwa kutokana na hatua yake ya kuenda katika mji Mtakatifu wa Makka kutekeleza ibada ya Umrah. Ozil ambaye pia ni mchezaji katika timu ya Ligu Kuu ya Uingereza ya Arsenal ni Mjerumani Mwislamu mwenye asili ya Uturuki.

Gauland amesema chama chake cha AfD kinaamini kuwa Uislamu hauna uhusiano wowote na Ujerumani na kwa hivyo hawaafiki mchezaji wa timu ya taifa kutekeleza ibada ya Umrah.

Kufuatia matamshi hayo, Ozil ameandika ujumbe katika mitandao ya kijami na kubaini kuwa hatasema zaidi isipokuwa kulaani matamshi hayo. Amesema kutoa jibu zaidi kwa Alexander kutamfanya mwanasiasa huyo apate itibari asiyostahiki.

Mwaka 2016 picha na video za Ozil akiwa mjini Makkah kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Umra zilienea katika mitando ya kijamii. Ozil ni kati miononi mwa wachezaji soka mashuhuri zaidi duniani.

Ozil amenukuliwa akisema kuwa kabla ya kuingia uwanjani katika kila mechi, yeye husoma aya kadhaa za Qur'ani.

3698791

captcha