Akihutubu katika sherehe za kufunga mashindano ya Qur'ani ya Jeshi la Kujitolea la Wananchi, Basij, mjini Tehran siku ya Jumamosi, kamanda huyo amesema mafanikio yaliyopatikana katika nyuga mbali mbali baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kutokana na kutekeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Halikadhalika amesisitiza kuwa, Jeshi la Basiji linapaswa kuwa mfano wa kuigwa na liwe ni lenye kutekeleza mafundisho ya Qur'ani katika setka mbali mbali. Amesema ili kufiukia lengo hilo kuna haja ya kuhifadhi Qur'ani na kutafakari kuhusu aya za kitabu hicho kitukufu.
Mashindano ya 25 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Jeshi la Basiji yalifanyika Tehran na washindi walitunukiwa zawadi katika sherehe zilizohudhuriwa na mkamanda wa ngazi za juu wa IRGC.