IQNA

Wanawake 7,000 katika Mashindano ya Qur'ani mjini Tehran

16:03 - December 09, 2017
Habari ID: 3471301
TEHRAN (IQNA)-Zaidi ya wanawake 7,000 wanashiriki katika awamu ya 11 ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani kwa wanawake mjini Tehran.

Mashindano hayo yanafanyika katika Kituo cha Darul Qur'an cha Imam Ali AS katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo yalianza Jumatano na yanatazamiwa kuendelea hadi Disemba 15.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mashindano hayo yatakuwa na makundi matatu ya mabarobaro (chini ya miaka 16) ,vijana (baina ya miaka 16-30)  na watu wazima (zaidi ya miaka 30).

Kategoria katika mashindano hayo zitajumuisha kusoma Qur'ani (tarteel) na kuhifadhi Qur'ani ambapo wenye kuhifadhi wanachagua mojawapo ya kategoria zifuatazo; kuhifadhi Juzuu 5, Juzuu 10, Juzuu 20 na Qur'ani Kamili.

Mbali na raia wa Iran pia kutakuwa na raia 318 wa nchi za kigeni waishio Iran wambao watashiriki katika mashindano hayo.

Mashindano hayo yamefadhiliwa kwa michango ya wanaharakati wa Qur'ani nchini Iran.

3670756

captcha