IQNA

Waislamu wanaoingia Marekani wapungua baada ya Trump

12:10 - July 13, 2017
Habari ID: 3471064
TEHRAN (IQNA)-Idadi ya Waislamu wanaoingia Marekani imepungua katika miezi mitano ya kwanza ya utawala wa Rais Donald Trump.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanya na taasisi ya utafitiya PEW Research wakati wa urais wa Barack Obama idadi ya Waislamu waliokuwa wakiingia Marekani kama wakimbizi ilikuwa kubwa lakini katika kipindi cha Trump Wakristo sasa ndio wanaoingia kwa wingi nchini humo kama wakimbizi.

Uchunguzi umebaini kuwa, kati ya wakimbizi wote walioingia Marekani baina ya Januari 20 alipoapishwa Trump na Juni 30, karibu nusu walikuwa Waislamu na asilimi 38 walikuwa Waislamu.

Ucunguzi huo ambao umechapishwa Jumatano umeonysha kuwa hadi kufikia Februari mwaka huu asilimia 50 ya wakimbizi waliokuwa wakiingia Marekani walikuwa ni Waislamu lakini hilo limebadilika.

Hayo yanajiri wakati ambao Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limesema idadi kubwa ya wakimbizi hutoka katika nchi zenye Waislamu wengi huku Syria ikiongoza kwa idadi kubwa ya wakimbizi.

Nchi zingine za Waislamu zenye idadi kubwa ya wakimbizini Somalia na Afghanistan. Hii ni katika hali ambayo, sera za kibeberu za nchi za Magharibi na hasa Marekani ndio chanzo cha vita na migogoro katika nchi hizo za Kiislamu.

Amri ya  Trump i inayowapiga marufuku raia wa nchi sita zenye idadi kubwa ya Waislamu kuingia katika ardhi ya Marekani imeanza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Juni baada ya kesi za mahakamani na upinzani mkubwa dhidi ya uamuzi huo.

Amri hiyo imawazuia Waislamu kutoka nchi za Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen pamoja na wahajiri kutoka nchi zote dunia kuingia Marekani katika kipindi cha siku 90 zijazo. 

Mtawala huyo wa kibaguzi wa Marekani,  alitoa amri hiyo miezi mitano iliyopita na kukabiliwa na upinzani mkubwa nje na ndani ya Marekani na hatimaye kusitishwa na mahakama za nchi hiyo zilizosisitiza kuwa, ni ya kibaguzi na kwamba inapingana na katiba ya nchi hiyo. Hata hivyo Mahakama Kuu ya Marekani imesitisha maamuzi ya mahakama nyingine za nchi hiyo na kuruhusu utekelezaje wake.

3618497


captcha